Watu 40 wakatwa mapanga huko Ituri Kongo

Watu wasiopungua 40 wameuawa katika shambulizi jingine la kutisha la wanamgambo wa ADF huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mpakani na Uganda. Inasemekana kwamba magaidi hao walitekeleza ukatili huo kwa kutumia mapanga na kwamba mbali na mauaji, wameiba pia vitu vya thamani vya wakazi wa kijiji hicho.

Mauaji hayo ya halaiki yameripotiwa siku moja baada ya wamgambo hao wa ADF kushambulia kijiji cha Makutano mkoani Ituru, karibu na Bunia, na kuua raia 17.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *