Ufaransa kuharibu maendeleo ya umoja wa Afrika

Mara nyingi maraisi wa Afrika wanajitahidi kutaka kuboresha bara hilo, ila katika nchi za tatu, maana yake Ulaya awako tayari kuona bara la Afrika linabadilika na kusonga mbele. Kilichojitokea siku hizi ni kwamba nchi za Afrika zilianza kuongea kwa pamoja kuanza mwaka wa 2003 kuhusu kuwa na pesa za pamoja kama vile Ulaya ilivyo na pesa za pamoja, ila kutokana kwamba nchi za Ulaya zinazo hamu ya kuona Afrika ikiendelea kurudi nyuma zinaendeleza kuweka ugumu ili kushawishi nchi zingine kukataa makubaliano hayo na kuweka pesa zaidi na zaidi. Swali linalobaki ni kwamba hivi wazungu wanataka bara la Afrika liendelee mbele ?

Mda uhu ambao nazungumza nawe msomaji wangu, katika Umoja wa Afrika kuko vikao vikubwa sana ambavyo vinaendelea ili kuweka pesa za pamoja kama alivyotaka shujaa mkuu, ayati Mohamed Kadafi ambaye alitaka Afrika iwe na pesa zake binafsi, ila hali ihi wazungu waliona mapema wakaingiza uchonganishi na kumuita kuwa dictator wa Libya, kuchonganisha wananchi na raisi wao kwakumwanga vijipesa ili wamuue shujaa huyo wa Libya. Ingawa huko Urusi kunasemekana kuwa Putin ni dictator ila hakuna atakayeweza kumfanya lolote lile. Haya nimeandika ila sijaamini kwamba Putin ni dictator ila imeonekana kwamba kila raisi ambaye anasemekana kuwa dictator maana yake huyo anafanya mambo ambayo maraisi wa ulaya awayafurahii.

Kinachohuma sana nikwamba baada ya nchi za Afrika kuwa kimoja na kuamua kuwa na pesa moja barani humo, Ufaransa imeingilia koloni zake za kifaransa ambazo ni Burkina faso, Mali, Niger, Senegal, Benin, Guinea Bisau, Ivory Coast na Togo kuwashawishi kuunda pesa za pamoja. Pesa hizo zitaitwa ECO ambazo zitakuwa katika nchi hizo 8 zilizo chini ya ukoloni wa Ufaransa. Cha kushangaza nikwamba nchi hizo zimesaini mkataba uho na Ufaransa na zimefurahi kwamba mapato ya nchi zao yatakuwa nachungwa nchi Ufaransa kwa asilimia 50. Ndungu msomaji unaelewa jinsi ghani Ufaransa inavyoendelea bado kukoloni nchi za Afrika mpaka leo? Imekuwa wapi kwamba pesa ao mapato ya nchi yako yachungwe katika nchi nyingine, na kwanini Ufaransa iendelee kuchukua pesa ao kuwa na share katika nchi za Afrika, kwanini viongozi wa Afrika awako makini? Hili linauma sana. Kwa Ufaransa kufanya hivi inaonesha kwamba nchi hiyo aitaki bara la Afrika liendelee. Na ndio maana nakuja kukubali msemo unaosemwa kwamba Afrika ikiwa na amani nchi za Ulaya zitageuka kuwa waomba omba, maana Ulaya aiwezi chochote bila kuiba na kunyanyasa Afrika kwa maendeleo ya nchi zao. Kama wewe ni zmalendo wa nchi yako naomba uyawazie hayo na ufunze watoto wako wanaokuja hali ihi labda siku moja wanaweza kuwa na mionekano tofauti na wakapigania uhu uonevu. Ebu basi niweke nanga hapa kwanza ili wakati mwengine nikuletee story nyingine ya uonevu wa Afrika.

Uhitaji kopy right ila usikose kuandika msg ihi umeitoa wapi.

You don’t need copyright, Just mention where you took the msg from

Mwandishi: Clovis

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *