KUAHIRISHWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI DR CONGO

Tume ya uchaguzi (CENI) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetangaza hapo jana tariki (03-01-2019) kupitia Corneille Nangaa kwamba uwezekano wakutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais siku ya Jumapili tariki 6 mwezi huu wenda isiwezekane kutokana na tatizo la vifaa (lojistiki).
Kutokana na tatizo hilo Nangaa hakueleza lini anafikiri matokeo hayo atayatangaza.

Kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi, matokeo yanaweza yakatangazwa hadi tariki 15 januari baada ya uchaguzi, naye rais atakayechaguliwa kuapishwa tariki 18 januari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *