UCHAGUZI WA RAIS NCHINI KONGO UMEKUWA MGUMU

Mashine za kupigia kura ziliaribika katika maeneo kadhaa na waangalizi walisema kuwa makosa yalikuwa yameonekana katika sehemu ya tano ya vituo vya kupigia kura. Karibu saa 5 jioni vituo vya kupigia kura vilipaswa kufungwa, lakini watu ambao tayari walikuwa kwenye mstari waliweza kupiga kura baadaye.
Katika uchunguzi wa hivi karibuni, uliyofanyika kabla ya uchaguzi, ulionyesha mgombea wa upinzani Martin Fayulu kuwa katika uongozi.

Matayarisho na uchaguzi havikupita vizuri, hiyo ndiyo hisia ya kwanza. Katika sehemu mbalimbali mjini Kinshansa kama vile nje ya Kinshasa, vyombo vya kupigia kura havikufika katika muda uliyopangwa, na sehemu zingine vifaa hivyo havikufika. Watu walitakiwa kukaa kwenye foleni ndefu kwa ajili ya kupiga kura ya kiongozi waliompenda kuchagua.

Masaa kadhaa baada ya kuanza uchaguzi, makumi ya vituo vya kupigia kura, vilikuwa bado kupewa karatasi za kupigia kura. Watu wawili wamefariki katika moja ya vijiji mashariki mwa nchi. Mauaji hayo yametokea wakati mtu mmoja aliposhikiliwa katika wizi wa kura. Polisi alimuua mwanaume mmoja katika vurugu hiyo na baadaye naye pia kufariki baada ya kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira.

Katika miji ya mashariki ya Kongo ya Beni na Butembo, uchaguzi ulifutwa na kuahirishwa rasmi mpaka machi. Serikali inasema imefanya hivyo kwa hofu ya kuzuka kwa Ebola. Lakini wakati huo huo, miji hiyo miwili ni ngome za upinzani, huku raïs atakayechaguliwa atahapishwa mwezi januari. Je, uchaguzi huo utayafuta matokeo ya rais atakayechaguliwa ?

Hakuna hali yoyote ya uaminifu katika uchaguzi, bali kuwepo uchaguzi huo ni kama ushindi wa raia dhidi ya Joseph Kabila ambaye kwa miaka miwili amesitisha uchaguzi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *